Thursday, December 30, 2010

no.2 TUKIO LILILONIFURAHISHA.....CHERRIE CO.LTD

Namshukuru sana Mungu,kwa kuniwezesha kusimama tena na kufungua kampuni yangu inayojihusisha na mambo ya filamu. Kuanzia 2011,wadau wangu kaeni tayari kupokea vitu vizuri toka CHERRIE CO.LTD kwa kuanzia tumeanza na BINTI NUSA ambayo pia tumeisambaza wenyewe. Kwangu si mara ya kwanza kuwa na kampuni,japo kuna ups and downs zilizojitokeza.lakini hii najivunia nayo zaidi,Kwani nimekuja kivingine kabisa.

Wednesday, December 29, 2010

no.3 TUKIO LILILONIFURAHISHA..........FILAMU YA BINTI NUSA


BINTI NUSA 1,2 & 3 Zimenifungia mwaka 2010.

Binti Nusa 1 ilitoka miaka miwili iliyopita,lakini ilipendwa sana, na watu walikuwa wanaiulizia kila mara.December hii nimewaletea mzigo huo part2 na 3,ambapo utakutana na mastaa wengi wakali SUSAN LEWIS,ELIZABETH CHIJUMBA,KENNETH AMBANI FROM KENYA,HASHIM KAMBI,MTANGA,NDUMBAGWE MISSAYO,FLORA MVUNGI,SHILOLE,na wengine wengi.

Imerekodiwa na Camera na vifaa vyenye ubora na vizuri zaidi,

Inafanya vizuri sana sokoni na natumai itaendelea kufanya vizuri.


Produced and Directed by YVONNE CHERRYL

no.4 TUKIO LILILONIFURAHISHA ..........................TUZO YA ZIFF MSANII BORA TOKA TANZANIA 2010

Napenda kushukuru MUNGU,Mama yangu,watoto wangu Sonia and Junior,My fans na wasanii wenzangu.Na hii TUZO ni YAKO WEWE!!Ahsante


VINCENT KIGOSI(RAY),JOYCE KIRIA(BONGO MOVIES SHOW),JANG'OMBE HEADMASTER,YVONNE CHERRYL,ISSA MUSA(CLOUD)AND STEVEN KANUMBA AT JANG'OMBE SECONDAY ZANZIBAR WHERE WE WENT TO VISIT DURING ZIFF






ZIFF(Zanzibar International Film Festival)hufanyika kila mwaka huko Ngome Kongwe,Zanzibar.likijumuisha filamu mbalimbali toka duniani,na mwaka huu ndio ulikuwa mwaka wa kwanza kuanzisha kitu kinachoitwa SWAHILI DAY ambapo filamu za kitanzania zilipata nafasi ya kuonyeshwa na kushindanishwa na kupigiwa kura ili kupatikana Filamu bora na Msanii bora,na pia walitualika mastaa wa filamu bongo na tukaenda kushiriki na kufanya kazi za jamii

Nashukuru Mungu kwa kushinda TUZO hiyo ya kwanza toka ZIFF.

Ila mwakani,msituchanganye wanawake na wanaume,nasuggest kuwe na TUZO ya msanii bora wa kike na wa kiume na FILAMU BORA.

Tuesday, December 28, 2010

no.5 TUKIO LILILONIFURAHISHA................76TH BIRTHDAY YA BIBI YANGU

My Bibi(RUTH JOSHUA) I love her so much.Bibi wa kizaramo aliyepandisha vidato,ungemkuta enzi zake zile za NYERERE...wewe!!!ungekoma naye,alikuwa anakimbiza sana...ha ha ha ha.

Yeye ndiye chimbuko langu,nampenda sana.Babu yangu ambaye ndiye aliyenipa jina la CHERRIE ambalo ni jina la kifaransa likimaanisha mpenzi,alifariki mwaka jana na bibi amebaki peke.

Ni mama wa mama yangu,ni rafiki yangu mkubwa na mshauri wangu mzuri sana.Mwaka huu tarehe 30 November ametimiza miaka 76,na tukamfanyia Party ndogo tu nyumbani kusherehekea pamoja naye.

Monday, December 27, 2010

NO.6 TUKIO LILILONISHTUSHA

Siku chache kabla ya Birthday yangu,wakati tunatoka kwenye Sherehe ya Kitchen Party ya rafiki yetu wa kanisani,mimi na mama yangu tulipata ajali.Ni kitendo cha dakika tu lakini kimedumu akilini mwangu hadi leo hii.Dereva aliyekuwa nyuma yetu alikuwa speed ya ajabu,na alipofika kwenye Roundabout ya Mlimani City, maeneo ya MWENGE,DAR ES SALAAM gari ilimshinda akaja kutugonga kwa nyuma nilipokuwa.gari yetu ikagonga ukuta wa barabara na kuzunguka kurudi tulipotokea,naye akaja tena kutugonga ubavuni,ubavu ule ule nilipokuwa nimekaa.Hatukuamini kama tumetoka salama,hakuna mtu aliyeumia japo mbavu na kichwa kiliuma sana kesho yake na ni kwa ajili ya mshtuko tu.Namshukuru sana MUNGU kwa kutuokoa katika ajali hiyo.Ni wengi wanaopata ajali na hawaponi,mimi ni nani nitoke mzima?Ni kwa REHEMA na MAPENZI yake MUNGU.



Naikumbuka sana siku hiyo,ilikuwa tarehe 8 ya mwezi wa 8.

Matokeo ya BORA ZA 2010 katika matandao wa FILMCENTRAL

Matokeo ya kura za waliofanya vizuri katika mwaka 2010, kutokana na mtandao wa FILMCENTRAL umeniweka katika nafasi ya mwigizaji bora wa kike 2010 bofya hapa

Sunday, December 26, 2010

No.7 TUKIO LILILONIFURAHISHA. MY FANS,FRIENDS AND FAMILY

Napenda kuwashukuru sana watu wa Media zote, marafiki zangu,ndugu zangu na mashabiki wangu toka pande zote za dunia. Mmekuwa faraja sana kwangu kwa mwaka huu wa 2010, hamkuniacha hata kidogo na mmendelea kuniweka hapa nilipo,Thank you.

Nimepokea zawadi nyingi sana mwaka huu kutoka kwenu, sio tu vitu bali hata mawazo yenu, kura zenu pale panapohitajika kufanya hivyo, salaam za kunitakia kheri, salaam za kunipongeza pale panapostahili kufanya hivyo, na pole pale nilipoumizwa, Nitake nini tena zaidi?

Sanura (Denmark)


Ahsante sana kwa fans wangu wa Facebook. Nawapenda
Ahsante kwa General Sanga in UAE kwa zawadi nzuri sana ya krismas
Ahsante kwa Sanura wa Denmark, hujanitupa
Habiba na Hawa,Dernmark Nawapenda
My Papa in Ghana, thanks for the Birthday Package...Was WOW!!!! Nakupenda
From Japan, Peter Ikongo and friends, thank you
Myovelwa Mfwaisa...ahsante sana.
Dina Marios from Clouds Radio, Nakupenda
Paster Myamba, You know I love you brother!
Hashim Kambi, sina cha kusema.


Vanitha Omary....Ahsante sana.
Lutheran wa UK.....thank u!
Credo and Gaza in Sweden,mpo?
Wadau wa Blog yangu, jamani Nawapenda sana.
Sheila Simba na Dj.Eddie wa Radio UHURU
Joyce Kiria Bongo Movies show
BINTI NUSA CAST & CREW...Thank u
Hybiscus Women Group...OH!!!
John Kitime...jamani sina la kusema.
KORISH FAMILY hamjui ninavyowapenda mmefanya kitu kikubwa sana katika maisha yangu.

Hawa (my pacha) mwaaaaaaaaaaaaa

My Pastor David Lutumba na Apostle Mary na wote wanaoabudu nami, ahsante kwa kuniombea.
Jamani Nawapenda sana sana tena zaidi ya sana.Tuendelee kuwa pamoja.....

Friday, December 24, 2010

no.8 TUKIO LILONIFURAHISHA.NDUMBAGWE MISSAYO

WEDDING DAY

VENUE:FLORIDA OYSTERBAY

COLOURS:BLACK & WHITE


PRE-WEDDING. VENUE: KILAMUU HALL MBEZI BEACH

COLOURS: YELLOW & GOLD


NDUMBAGWE'S DRESS: By NATASHA WA MITINDO


KANUMBA AND I AT THE WEDDING

MY DRESS FROM WEST AFRICA

NDUMBAGWE AND I


WITH MY FRIEND DOROTHY

KITCHEN PARTY

VENUE: VIJANA HALL ,KINONDONI

COLOURS: BROWN & ORANGE(KITENGE)

MY DRESS: By NATASHA WA MITINDO





ENGAGEMENT DAY

VENUE: NDUMBAGWE'S HOME


NDUMBA AND I DRESSED By NATASHA WA MITINDO


Ndumbagwe Missayo aka THEA ni zaidi ya rafiki kwangu, mimi kwangu ni ndugu yangu kabisa. Ninampenda sana, na ndoto yake kwa muda mrefu ilikuwa ni kupata mtu wa kumuoa. Na nimefurahi kwamba MUNGU amemjaalia amempata mwenza wake Mwaka huu, MIKE SANGU. Harusi yake ilifungwa tarehe 6 November 2010, lakini safari yake ya kuelekea siku hiyo ilianza mapema mwaka huu. Na haya ndiyo matukio ya safari yake hiyo ya kusema "I DO"

NO 9.TUKIO LILILONIFURAHISHA

Filamu ya NIMEOKOKA ndiyo iliyonifungulia mwaka huu 2010. PASTOR DAVID LUTUMBA aliponiita kwa ajili ya kufanya filamu hii nikajua tu kwamba huo ni mwazo mzuri wa MWAKA WENYE MAFANIKIO. Filamu inamuhusu mwanamke aliyeokoka (YVONNE CHERRYL) na mwenye Imani kali juu ya wokovu wake japokuwa MUME wake (PASTOR JIMMY KAPEND) na baba yake (PASTOR DAVID LUTUMBA) walikuwa ni kikwazo kikubwa juu ya wokovu wake.Lakini mwisho wa siku MUNGU akamuokoa baba na mume wake katika MAPITO makubwa waliyoyapitia.
Filamu imetayarishwa na RIVER OF LIFE MINISTRIES,chini ya KANISA la MLIMA WA MABADILIKO,ambako ndipo ninapoabudu.Na hizi ni picha za UZINDUZI WA FILAMU HIYO uliyofanyika LAMADA HOTEL,DAR ES SALAAM
UPENDO NKONE hakuwa mbali katika kutumbuiza kwenye UZINDUZI huo, HUKU NA HUKO KAMA MAWIMBIIIIIIII
LUMOLE MATOVOLWA(BIGGIE) mmoja wa waigizaji wa filamu ya NIMEOKOKA
PASTOR JIMMY KAPEND, na mke wake PASTOR ANGEL
DVD ya nimeokoka inavyoonekana
APOSTLE Mary Lutumba








Thursday, December 23, 2010

MATUKIO 10 YALIYONIFURAHISHA NA KUNIHUZUNISHA KWA MWAKA HUU WA 2010






2011 is around the corner. Kuna mambo mengi mazuri,na mabaya ambayo yamenitokea katika maisha yangu na watu wangu wa karibu kwa mwaka huu wa 2010. Wakati siku chache tu zikisalia,kuukaribia mwaka huo mpya, nitawaletea matukio 10 ambayo kwangu yalinifurahisha na kunisikitisha.

Leo tuanze na Namba 10.

SONIA AKINYI..8 YEARS
My first born,amenifurahisha sana kwa mwaka huu, amefanya vizuri sana darasani lakini pia amefanya vizuri katika kazi mbalimbali za MATANGAZO YA TV, hadi mimi mwenyewe nikashangaa. Amefanya vizuri kwenye tangazo la magodoro ya COMFY, lakini pia amefunika na kuacha gumzo kwenye tangazo la VODA alipoachia ule usemi wa "HII GARI YA MAMA''Am proud of you My daughter,and Mammy loves you so so much.

Saturday, December 11, 2010

CHIKI MCHOMA'S BIG DAY AT MSASANI BEACH CLUB. THE COLOURS OF THE WEDDING WERE RED & GOLD

  1. MAHSEIN AWADHI(DR.CHENI) WITH HIS CHARMING WIFE. HE WAS THE MASTER OF CEREMONY OF THE WEDDING.
MIKE SANGU, (NDUMBAGWE MISAYO'S HUSBAND) AND I, MY DRESS WAS MADE BY MY MAMA-NATASHA WA MITINDO
NDUMBAGWE MISAYO (THEA),WHO PLAYED THE PART OF INSPECTOR OF POLICE IN THE FILMS BINTI NUSA1,2,&3 WHICH IS OUT NOW
BRIDE AND GROOM.CHIKI IS AN ACTOR AND THE CHAIRMAN OF KAOLE SANAA GROUP

CUTTING AND SHARING NDAFU

Tuesday, December 7, 2010

BONGO MOVIES JUMATANO SAA 3.30 USIKU, BINTI NUSA


MONALISA AND OTHERS ON EATV,BONGO MOVIES SHOW THIS WEDNESDAY 8TH AT 9.30 PM.PLZ DONT MISS TO WATCH THE MAKING OF BINTI NUSA.....
MONALISA AKIWA NA WASHIRIKI WENGINE WATAKUWA KATIKA KIPINDI CHA BONGO MOVIES JUMATANO TAREHE 8, SAA 3 NA NUSU USIKU, USIKOSE KUANGALIA JINSI BINTI NUSA ILIVYOTENGEZWA.