Tuesday, January 10, 2012

filming ya Trailer ya BLEEDING SUNSHINE.. ACCRA,GHANA



BLEEDING SUNSHINE Filamu ya kiafrika itakayoshirikisha mastaa wa Hollywood,hapa tulikuwa tunashoot trailer yake huko Accra,kwa akina Majid Michel,John Dumelo,Nadia Buari,Jacki Appiah na mastaa kibao wa nchi hiyo.






D.O.P,Director of photography wa filamu hiyo kutoka Hollywood,CHASE BOWMAN na 2nd Asst.DOP wake wakiwa mzigoni




Ha ha ha Tigo jamani Tigo kah!na yenyewe inataka kuuza sura



Hiyo scene ilikuwa ya shule,usishangae kuona wanafunzi wengi.ni kushangaa tu!nani amekuambia Buguruni tu ndio watu wanashangaa Hata kwao hivyo hivyo ha ha ha


Hao ni mastaa wa Ghana waliokuwa wakicheza kama wanafunzi katika Scene hiyo.Yule pembeni mama mjamzito ndiyo mtayarishaji na muongozaji wa filamu hiyo.Mzaliwa wa Ghana,Raia wa Marekani anayefanya kazi huko Hollywood anaitwa Yaa Boa Anning.
Nilienjoy sana kipindi chote cha Production hiyo na kujifunza vitu vingi vipya lakini kikubwa pia kujifunza lugha tofauti za nchi hiyo lakini neno rahisi ambalo hata wewe utalishika kirahisi sema AKWAABA.....linamaanisha KARIBU.Imetulia eh?

Sunday, January 1, 2012

BONGO MOVIES BEACH PARTY 2011


from right:Jack wolper,Ummy aka Dokii,na mimi mwenyewe

Kila mwisho wa mwaka,kampuni ya usambazaji wa Filamu nchini STEPS hufanya beach party ya kufunga mwaka na kuwashukuru wasanii na watayarishaji wa filamu ambao wamefanya nao kazi.
 Jacob Stephen ambaye tumetoka naye mbali sana tangu enzi za mambo hayo,unakumbuka?naye bila kukosa.

 Susan Lewis aka Natasha aka Mama yangu,ha ha ha hiyo ya pili sio aka bwana.....mama yangu kipenzi naye apitwe?

 From left:Jenifa Kyaka aka Odama,Me,na Mayasa Mrisho aka Maya

 Mkurugenzi wa Steps Entertainment Ltd Mr.Dilesh akinikabidhi Certificate of Appreciation iliyosomeka THERE'S NO S-CCES WITHOUT U!Imetulia

 Tukipiga story kidogo na bibie Salama Salmin aka Sandra huku vikuku vikipanda kwa mbali,umekosaje?

Mwisho mzee wa Relax akinipa shavu,ha ha ha Peter Msechu naye aliyekuwepo

Party ilifanyika Sunrise Beach Hotel Kigamboni.Ilikuwa Party nzuri kwakweli,Inafrica Band ilikuwepo na vikundi mbalilmbali kuachilia mbali watayarishaji wote wa filamu Tanzania unaowafahamu.