Friday, December 24, 2010

NO 9.TUKIO LILILONIFURAHISHA

Filamu ya NIMEOKOKA ndiyo iliyonifungulia mwaka huu 2010. PASTOR DAVID LUTUMBA aliponiita kwa ajili ya kufanya filamu hii nikajua tu kwamba huo ni mwazo mzuri wa MWAKA WENYE MAFANIKIO. Filamu inamuhusu mwanamke aliyeokoka (YVONNE CHERRYL) na mwenye Imani kali juu ya wokovu wake japokuwa MUME wake (PASTOR JIMMY KAPEND) na baba yake (PASTOR DAVID LUTUMBA) walikuwa ni kikwazo kikubwa juu ya wokovu wake.Lakini mwisho wa siku MUNGU akamuokoa baba na mume wake katika MAPITO makubwa waliyoyapitia.
Filamu imetayarishwa na RIVER OF LIFE MINISTRIES,chini ya KANISA la MLIMA WA MABADILIKO,ambako ndipo ninapoabudu.Na hizi ni picha za UZINDUZI WA FILAMU HIYO uliyofanyika LAMADA HOTEL,DAR ES SALAAM
UPENDO NKONE hakuwa mbali katika kutumbuiza kwenye UZINDUZI huo, HUKU NA HUKO KAMA MAWIMBIIIIIIII
LUMOLE MATOVOLWA(BIGGIE) mmoja wa waigizaji wa filamu ya NIMEOKOKA
PASTOR JIMMY KAPEND, na mke wake PASTOR ANGEL
DVD ya nimeokoka inavyoonekana
APOSTLE Mary Lutumba








No comments:

Post a Comment