Tuesday, November 8, 2011

PALE FILAMU ZINAPOTURUDISHA DARASANI

Unaweza kuhisi kwamba pindi unapovaa joho ama la kuhitimu kidato cha nne cha sita ama joho la heshima la chuo kikuu kwamba umemaliza kila kitu kuhusu kusoma dah!!! katika tasnia ya filamu mambo yanarejea kulekule kusoma kama kawaida. halafu mbaya zaidi ukiwa muhusika mkuu kuna kitu kinaitwa SCRIPT wanaoifahamu lugha vizuri wanasema ni mswada,mh!! yaani hapo ni zaidi ya darasa,kama ulikuwa hauna mazoea ya kukaririri 'what is biology,what is civics' sasa huku hakuna ujanja lazima ukaririri kwanza ndo uende mbele ya kamera,halafu huku hakuna cha kuangalizia ukithubutu kuangalizia kamera inakuumbua kwa hiyo lazima ukariri,aliyekwambia unaweza kuielewa script nani??? labda kama hiyo filamu umetunga mwenyewe kichwani,asikwambie mtu jamani script haina cha mzoefu

Hapa kama script inamzingua vile Monalisa,lakini sasa atafanyaje na ndo hiyo ajira yake na huyu mama yangu naye anaandaa hapo script kazi kwenye kukariri halafu mkononi ana pesa dah! sijui mchaga.




"mh!!! mona mbona kama siielewi hii sehemu" anaonekana kusema bi. Natasha huku Monalisa akimtazama nadhani hapo anamshangaa mama yake kwani kalazimishwa kuwa msanii,yaani script haina cha mkongwe wala under ground.

Endeleeni tu kunifanyia make up lakini script siachii" anasema mwanadada Lucie Komba hapa akiwa anasubiriwa kwenye kamera dah!! kumbe usanii kazi eeh!!!

hapa hata ladha ya hicho kinywaji huwezi kupata kama bado hujameza mistari yako katika script

inafikia wakati unaweza ukalia maana utamsikia director take one,take two,take three he mara anafikia take five dah!! kila saa eti umekosea script lazima ulie hapa mama alizingua katika kumeza kaneno flani hivi

huku script hujameza vizuri mnaelekea location mara na gari linawaharibikia

hapa hakuna ujanja we Mona utashika jeki na Lucie Komba atashika spana

lakini mwisho wa siku mmemaliza kushoot kifuatacho ni tabasamuuuuu

1 comment: