Saturday, March 5, 2011

Nimetembelea Kambi ya Yatima na Wazee wasiojiweza na kula lunch pamoja nao


Nungwi-Kigamboni kwenye kambi ya yatima na wazee wasiojiweza zamani ikifahamika kama kambi ya wenye Ukoma ndiko nilipotembelea weekend hii na kula lunch pamoja nao.Chakula kilichopikwa na sisi wenyewe katika kikundi chetu cha wanawake cha Hybiscus



Hapa tukipata msosi na kupiga story mbili tatu na bibi huyu ambaye ni mgonjwa na anayeishi kambini hapo,alifurahi sana.


Chakula bila maji?Nikiwahudumia watoto



Huyu mtoto alinitia majonzi na kunidondosha chozi....Ni yatima na hapo kambini yupo yeye na wadogo zake wawili.Alinipenda sana nami nimempenda sana pia



Akiendelea kunielezea mkasa wake


ITS TIME TO GO,Tukawaachia na zawadi ndogo ya vyakula tulivyojaaliwa kununua.michele,unga,mafuta,sabuni na vitu kama hivyo ili viweze kuwafariji na kufahamu kuwa kuna watu mahala fulani ambao tunaguswa kwa namna moja au nyingine na matatizo yao.