Monday, December 26, 2011

MIAKA 20 KATIKA GAME BILA KUCHUJA,LUNDO LA TUNZO!!!

Ana miongo miwili katika tasnia ya filamu hapa nchini akiwa amepiga hatua hadi nje ya Tanzania, mbali zaidi ameusogeza mguu wake mmoja katika dreamland ya wa sanii wengi,"kuingia Hollywood".
Ameianza tasnia hii tangu akiitwa mtoto, baadaye msichana halafu hadi sasa anapoitwa mzazi bado anapeta katika game hili.
Kampuni inayozalisha magazeti pendwa ya burudani hapa yaani Global publishers nchini ililithibitisha hili kwa umma baada ya kufanya shindano baab kubwa lililowapambanisha wakali mbalimbali katka fani mbalimbali za saana hapa nchini, ni kura ya msomaji ilikuwa inaamua mshindi ni nani.
HAPA AKIWA MZIGONI si unajua kwama ana taaluma ya kuongoza filamu!!!!!!
HALAFU HAPA AKIWA MAMA......na mtoto wake wa mwisho kwa sasa
Kama kura zilipigwa na msomaji basi mwanadada Yvonne Cherryl Monalisa anakubalika ile sana, amefunika mastaa wote wa kike ambao ni maarufu na kuingia katika kumi bora ya kuwania tuzo zinazotolewa na kampuni hiyo ya Global Publishers zinazokwenda kwa jina la Tanzania Walk Of Fame. Katika orodha hiyo wanaume ni wanne na Monalisa akiungana na Jaydee,Bi. Kidude, na Rose Mhando katika kundi la wanawake wanne wa shoka hapa Bongo linapokuja suala la kuitunza Nyota ya umaarufu.

Thursday, December 22, 2011

POLENI KWA MAFURIKO TANZANIA

Ni jambo la kusikitisha sana lakini yote ni mipango ya Mungu huu si wakati muafaka wa kuwalaumu waliojenga mabondeni licha ya kupewa maonyo mara kwa mara bali ni wakati wa kuangalia nini tunafanya

hizi ni baadhi ya sehemu.......unaweza kuamini hapa ni barabarani???? yeah!! kama we ni wa hapa Dar na ulikuwa katika mizunguko ya hapa na pale siku ya jana na juzi waweza kuwa shahidi.
 kama utani vilelakini huu ndio ukweli ilivyokuwa jana hapa jijini.......wamepoteza makazi hao tayari,serikali!!!!!!!! wapiga kura wenu hao,lakini na wewe mtanzania jirani yako huyo

Sunday, December 11, 2011

PIC OF THE WEEK

Location:Kinondoni,Studio
Dar es salaam
July,2011

Jamani hapo ilikuwa ni Photo Shoot kwa ajili ya cover ya muvi ya Emanuel Myamba huyo hapo pichani,Muvi imeshatoka ipo sokoni kwa hivi sasa inaitwa PASTOR MYAMBA-THE TRIALS 1& 2,
Myamba ni kati ya wasanii wakali wa Bongo,anayefanya vizuri sana katika filam mbalimbali na kwa sasa ameanzisha chuo cha filamu....Haya sasa kazi kwenu kwa wapenda kusomea sanaa mnakaribishwa.

Thursday, December 8, 2011

TOGOOOOOOOOO!!!!!

 Togo,West Africa
 May,2011

Togo,small country but very beautiful.Nilienjoy kwakweli.Wish to go back there soon.


 Ni mkoko tu uliokuwa ukinizungusha hapa na pale ili mradi niutumie muda wangu vizuri wakati natalii katika nchi hiyo.

Mwisho wa siku,maua yana sehemu yake bana.beautiful flowers kwa beautiful lady,au sio?ha ha ha

Friday, December 2, 2011

MAMBO YA KONOKONO!!

MADINA MARKET,GHANA.
April,2011.

Inaitwa  tembea uone,duh!nilikuwa nasikia tu kwamba jamaa wa Afrika Magharibi wanakula konokono nikataka kuona kwa macho yangu mwenyewe.Si ndio nikatia timu katika soko la Madina,huko Ghana kujionea.Hapo ni kama nataka kukimbia,wenyeji wangu wacha wacheke.

 Jamaa ndio haooooo,wanatembea tembea kwenye beseni.kilichonishangaza yani wanauzwa very expensive eti hako kakonokono kamoja ni karibu buku 5 ya kibongo...loh!

Nyama nyama nyama?nyamaaaaaa

Thursday, December 1, 2011

TUKO PAMOJA NAWE SAJUKI NA FAMILIA YAKO

Timu nzima ya Monalisafilms blogspot inaungana na watanzania na wasiokuwa watanzania lakini wanaofahamu fika hali ya kiafya ya msanii wa maigizo Juma Kilowoko al-maarufu kama Sajuki katika kipindi hiki kigumu sana,pamoja tunakuombea upone haraka na kurejea katika shughuli zako za kila siku.Maombi yetu pia kwa mama Sajuki (Wastara),Mungu akutie nguvu katika kipindi hiki cha kumuuguza mumeo.

Kutoa ni moyo kwa yeyote mwenye chochote kitu kwa nia moja ameamua kumfariji mgonjwa awasiliane na blog hii ya Monalisafilms kwa namba 0718958758 ama email yvonnecherryl@gmail.com na mchango wako utafikishwa mahali husika..