Monday, October 31, 2011

TUWE SAUTI YAO



Naamini hawawezi kusikika hata wakizipaza sauti zao juu sana,si tu kwa sababu sauti zao ziko chini HAPANA ila watanzania wameziba masikio yao wasiweze kuwasikia na kuwasaidia.
Hebu kuwa wa kwanza kufungua masikio yako na kumsikikliza bibi huyu akilia kwa uchungu mkali analia kilio cha upendo,upendo wake unasababisha chozi lake limdondoke. Hana uwezo mkubwa sana lakini ana upendo,kipato chake ni duni lakini bado anahitaji kusaidia wengine,kubwa zaidi ni MLEMAVU lakini hilo halimkatishi tamaa,kutana na bibi huyu katika show malidhawa itakayokujia hivi karibuni
. Je unaamini kwamba waweza kuwa mlemavu lakini bado ukawasaidia wengine wasiojiweza zaidi yako??

"mabadiliko huanzia kwa mmoja na hatimaye dunia nzima" anaonekana akisema mama huyu mlemavu ambaye ana jukumu linalomzidi uzito....vuta subira utamfahamu kiundani hivi karibuni.......

Thursday, October 20, 2011

MONALISA KUISHANGAZA TANZANIA NA DUNIA!!!

Msanii maarufu wa filamu hapa nchini anayewika hadi nchi za watu huku akijivunia kuwa muigizaji bora wa kike kipindi flani hivi sasa anakuja kivingine kuikamata Tanzaniana mipaka yake.....unahisi anaandaa filamu mpya bada ya kutamba naBinti Nusa iliyompa tunzo??...au unadhani anaandaa muziki???...mimi na wewe hatufahamu kama ndo ameamua kuacha sanaa ya filamu ili kuishangaza Tanzania au vipi,yeye mwenyewe hakufunguka sana ila alisema kaneno flani hivi nami namnukuu
"coming soooon!!!!!!" hebu tazama hapa akiwa bize nyuma ya camera katika hizo location hapa juzi kati.

hapa mama na mwana...Monalisa akiwa anaandika masuala kadhaa soon baada ya kufika location.

I AM BACK


Ni siku nyingi sana nimekuwa kimya katika ulimwengu huu wa blogu lakini sasa nimerejea mzima mzima kuendelea kuwa nanyi karibu,kuwajuza nanyi kunijulisha mambo kadha wa kadha katika tasnia hii ya filamu zetu za kibongo. Fuatana nami upya tena kama zamani........hebu ngoja niwapigie namba zenu kama mnapatikana maana na nyie kwa kubadili namba siwawezi