Monday, December 26, 2011

MIAKA 20 KATIKA GAME BILA KUCHUJA,LUNDO LA TUNZO!!!

Ana miongo miwili katika tasnia ya filamu hapa nchini akiwa amepiga hatua hadi nje ya Tanzania, mbali zaidi ameusogeza mguu wake mmoja katika dreamland ya wa sanii wengi,"kuingia Hollywood".
Ameianza tasnia hii tangu akiitwa mtoto, baadaye msichana halafu hadi sasa anapoitwa mzazi bado anapeta katika game hili.
Kampuni inayozalisha magazeti pendwa ya burudani hapa yaani Global publishers nchini ililithibitisha hili kwa umma baada ya kufanya shindano baab kubwa lililowapambanisha wakali mbalimbali katka fani mbalimbali za saana hapa nchini, ni kura ya msomaji ilikuwa inaamua mshindi ni nani.
HAPA AKIWA MZIGONI si unajua kwama ana taaluma ya kuongoza filamu!!!!!!
HALAFU HAPA AKIWA MAMA......na mtoto wake wa mwisho kwa sasa
Kama kura zilipigwa na msomaji basi mwanadada Yvonne Cherryl Monalisa anakubalika ile sana, amefunika mastaa wote wa kike ambao ni maarufu na kuingia katika kumi bora ya kuwania tuzo zinazotolewa na kampuni hiyo ya Global Publishers zinazokwenda kwa jina la Tanzania Walk Of Fame. Katika orodha hiyo wanaume ni wanne na Monalisa akiungana na Jaydee,Bi. Kidude, na Rose Mhando katika kundi la wanawake wanne wa shoka hapa Bongo linapokuja suala la kuitunza Nyota ya umaarufu.

Thursday, December 22, 2011

POLENI KWA MAFURIKO TANZANIA

Ni jambo la kusikitisha sana lakini yote ni mipango ya Mungu huu si wakati muafaka wa kuwalaumu waliojenga mabondeni licha ya kupewa maonyo mara kwa mara bali ni wakati wa kuangalia nini tunafanya

hizi ni baadhi ya sehemu.......unaweza kuamini hapa ni barabarani???? yeah!! kama we ni wa hapa Dar na ulikuwa katika mizunguko ya hapa na pale siku ya jana na juzi waweza kuwa shahidi.
 kama utani vilelakini huu ndio ukweli ilivyokuwa jana hapa jijini.......wamepoteza makazi hao tayari,serikali!!!!!!!! wapiga kura wenu hao,lakini na wewe mtanzania jirani yako huyo

Sunday, December 11, 2011

PIC OF THE WEEK

Location:Kinondoni,Studio
Dar es salaam
July,2011

Jamani hapo ilikuwa ni Photo Shoot kwa ajili ya cover ya muvi ya Emanuel Myamba huyo hapo pichani,Muvi imeshatoka ipo sokoni kwa hivi sasa inaitwa PASTOR MYAMBA-THE TRIALS 1& 2,
Myamba ni kati ya wasanii wakali wa Bongo,anayefanya vizuri sana katika filam mbalimbali na kwa sasa ameanzisha chuo cha filamu....Haya sasa kazi kwenu kwa wapenda kusomea sanaa mnakaribishwa.

Thursday, December 8, 2011

TOGOOOOOOOOO!!!!!

 Togo,West Africa
 May,2011

Togo,small country but very beautiful.Nilienjoy kwakweli.Wish to go back there soon.


 Ni mkoko tu uliokuwa ukinizungusha hapa na pale ili mradi niutumie muda wangu vizuri wakati natalii katika nchi hiyo.

Mwisho wa siku,maua yana sehemu yake bana.beautiful flowers kwa beautiful lady,au sio?ha ha ha

Friday, December 2, 2011

MAMBO YA KONOKONO!!

MADINA MARKET,GHANA.
April,2011.

Inaitwa  tembea uone,duh!nilikuwa nasikia tu kwamba jamaa wa Afrika Magharibi wanakula konokono nikataka kuona kwa macho yangu mwenyewe.Si ndio nikatia timu katika soko la Madina,huko Ghana kujionea.Hapo ni kama nataka kukimbia,wenyeji wangu wacha wacheke.

 Jamaa ndio haooooo,wanatembea tembea kwenye beseni.kilichonishangaza yani wanauzwa very expensive eti hako kakonokono kamoja ni karibu buku 5 ya kibongo...loh!

Nyama nyama nyama?nyamaaaaaa

Thursday, December 1, 2011

TUKO PAMOJA NAWE SAJUKI NA FAMILIA YAKO

Timu nzima ya Monalisafilms blogspot inaungana na watanzania na wasiokuwa watanzania lakini wanaofahamu fika hali ya kiafya ya msanii wa maigizo Juma Kilowoko al-maarufu kama Sajuki katika kipindi hiki kigumu sana,pamoja tunakuombea upone haraka na kurejea katika shughuli zako za kila siku.Maombi yetu pia kwa mama Sajuki (Wastara),Mungu akutie nguvu katika kipindi hiki cha kumuuguza mumeo.

Kutoa ni moyo kwa yeyote mwenye chochote kitu kwa nia moja ameamua kumfariji mgonjwa awasiliane na blog hii ya Monalisafilms kwa namba 0718958758 ama email yvonnecherryl@gmail.com na mchango wako utafikishwa mahali husika..

Monday, November 28, 2011

POLE SANA YUSUPH!!!




 YUSUPH MLELA akiwa na Marehemu baba yake MR..MLELA




Yusuph Mlela,moja kati ya mastaa wakali wa muvi za kibongo,amefiwa na baba yake mzazi pichani hapo juu leo.Kwa niaba ya mafans wangu wote toka pande zote za dunia nachukua nafasi hii kukupa pole sana kwa kumpoteza kipenzi chako.Tupo pamoja nawe katika kipindi hiki kigumu,tunakuombea kwa Mungu ili akupe nguvu za ziada za kushinda maumivu unayoyasikia sasa.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA,JINA LAKE LIBARIKIWE.

Saturday, November 26, 2011

PIC OF THE WEEK

Kalsoume Sinare and I,Accra-Ghana.March,2011

Kalsoume Sinare,ni mmoja kati ya waigizaji wakongwe na mahiri wa Ghallywood.Yeye ndiye alikuwa symbol yangu kwa miaka ya nyuma katika kufahamu kwamba hii ni filamu ya ghana.Amekuwepo kwa muda mrefu sana,tangu alikuwa akicheza kama kasichana,na sasa bado anaendelea kukimbiza tu.

Mara yangu ya kwaza kabisa kutia maguu Accra,yeye ndiye mtu wa kwanza nilliyekuwa nawish kummeet na kubadilishana naye mawazo mawili matatu kuhusiana na kiwanda cha filamu sio Bongo wala cha Ghana,bali kiwanda cha filamu Africa.Ni ndoto yangu kuona siku moja Producer wa Nollwood anapoandaa filamu anaanza kufikiria Cast kutoka Angola,au Rwanda.Producer wa Bongo anamfikiria msanii wa Ghana au South Africa,Producer wa Ghana anamfikiria msanii wa Kibongo au Burundi,INAWEZEKANA.

I was so excited kukutana na Kalsoume Japo kwa bahati mbaya hakuwa wa kwanza tena kukutana naye kama ilikvyokuwa ndoto yangu kwani nilishakutana na MAJID MICHEL, na ADJETEY ANANG.Lakini Kalsoume alinipokea vizuri sana,ni mcheshi na mkarimu.Nilienjoy kwa kweli,na akaniinvite dinner mara nyingine nitakayokuwa huko,japo niliporudi tena in Sept..i was so busy na mambo mengine hatukuonana.

Kalsoume ni mke na mama wa watoto wawili wa Kiume.

Habar toka News One-Accra,Ghana

Monday, 21 November 2011

Bleeding Sunshine: A Hollywood Thriller On Human Trafficking Begins In Accra





It has become evident that female movie makers from Africa have taken the continent’s movie industry a step further in recent times.
Chineze Anyaene’s ‘Ije’ and Leila Djansi’s ‘Sinking Sands’ are a few classic examples. 
The world is about to witness another landmark achievement in the history of movies as an American-based Ghanaian female filmmaker, Yaa Boaa Aning, parts the curtains for ‘Bleeding Sunshine’, an international standard feature film on human trafficking.
Yaa has just wrapped up the Ghana shoot of the film but would take shots from some other significant locations in Egypt, Dubai and Israel.
‘Bleeding Sunshine’ sheds light on the untold intricacies of human trafficking with emphasis on African teenagers trafficked to other parts of the world, particularly to Europe for mostly commercial sexual exploitation.
It significantly tackles some of the modus operandi of traffickers while sharing firsthand information on what victims go through. 
This brings to bare the nightmares of a young Ghanaian girl, played by Suzzy Nabor, who was adopted from her humble fishing village and thrust into the gritty world of international human trafficking.
Yaa Boaa Aning wrote the film’s script five years ago when she was doing a research on Interpol. Through the research, she came across an article which inspired her to carry further investigation into human trafficking issues.
Yaa Boaa, a Bachelor’s degree holder from the University of North Carolina at Chapel Hill, who has worked in Hollywood for the last 10 years, is fascinated by the beautiful locations in Ghana and stated that it was one of the factors that inspired the feature.
“I mean it is so beautiful out here. Part of the reasons to shoot was to show Ghana in a way it has never been shown before to the world before. There is going to be photo-tourism. Everywhere we turned our camera there is richness of culture and we want people in abroad to see and remind people that leave here how special this place is and also inspire them to look after it,” she told NEWS-ONE.
“There were certainly some challenges that I did justice to. But I mean the benefit is just how great the locations are here. We shot in Prampram and the abandoned Polo Club with the view of ocean with horses running in the background. We also did a number of sunrise shots, with fishermen pushing their boats out into the ocean and the sun coming up behind them. There are incredible scenes out there that I don’t get to see in Hollywood. You know it is something so different. It is really great. The pictures have never been done before,” added Chase Bowman, Director of photography (DOP) of Bleeding Sunshine.
Chase is a top Hollywood DOP with film credits like ‘Excuse Me For Living’ featuring Tom Pelphrey, Christopher Lloyd, Robert Vaughn, Wayne Knight, Jerry Stiller and Dick Cavett; the Warner Bros. release ‘Listen To Your Heart’ featuring Cybil Shepherd and Ernie Sabella; ‘In a Pickle’ starring Jackie Mason, and ‘Cost of a Soul’, which was theatrically released nationwide at 50 AMC theaters in April 2011.
He started shooting professionally at the age of fourteen, refined his skills by studying art and photography in Rome, and ran his own production company for ten years. His involvement in ‘Bleeding Sunshine’ is his first experience working in Ghana and second in Africa after his previous job in Kenya.       
With heart-throbbing scenes, the story of ‘Bleeding Sunshine’ is told with a great cast from around world; one reason the movie is expected to sell internationally.
Although Hollywood cast are to be made public, the film’s African cast will include 2007 ‘Pirates of the Caribbean’ star Hakeem Kae-Kazim, Omar Sheriff, Amonobea Dodoo, Steven Kanumba, 2011 Pan African best Actor- Chris Attoh, 2010 Zanzibar Intl Film Fest Award Best Actress-Yvonne Cherryl from Tanzania, and 2010 Africa Movie Academy Awards (AMAA) Best Actor, AdjeteyAnang (Pusher).
 AMAA 2011 Best Actress - Ama K Abebrese, Suzzy Nabor, Jasmine Baroudi of ‘Adams Apples’ fame, Lady Arafua, R&B sensation Katou and Lucy Kwao and others are part of the cast.
“I played the character of Captain Addo, a fisherman, the father of Suzzy, the little girl who was trafficked overseas. But I have shot lifespan in it. It is great production and very professional. I was always on my toes because I knew that I have to raise my level. It wasn’t a layback experience or like what we have back home. The director and crew were down to earth; I can’t pinpoint anything I didn’t like about this production,” Adjetey Anang said about his role in the project.
Yaa Boaa hoped the film would be the next big thing on the international movie scene when it was finally done.  
Yaa Boaa, born to Ghanaian parents in the US some years ago, has made a name in USA for her enormous contributions in US entertainment industry.
She started her career in advertising in New York. But bored with the lack of creative expression in account management, she decided to try her hands at fashion show production with some of the most prominent houses in the world- Giorgio Armani, BCBG, Jeremy Scott, and Betsey Johnson to name a few.
Fashion show production lead to fashion styling, which lead to film costuming, which ultimately exposed her to the enduring art of filmmaking, working with such acclaimed directors as Michael Mann, Bill Condon and John Singleton. Never letting go of her passion for writing, between 2007 and 2010, Yaa Boaa completed her first 5 feature scripts.
In 2009, she wrote and directed award-winning short film, ‘The Prince of Venice’.  Other projects include ‘Felix Triangle for President,’ which is currently in pre-production and ‘Zahara’ which is in postproduction.
Yaa is known for production roles in Hollywood movies and television series such as ‘Fast & Furious’,  ‘Bolden’, ‘Forcing the Blues’, ‘The Goods: Live Hard, Sell Hard’, ‘Deep in the Valley’, ‘Fashion Rocks’, ‘Feast’, ‘xXx: State of the Union’, ‘Just Legal’, ‘Flight of the Phoenix’, ‘Stuck on You’, ‘Out of Time’ and ‘Private Practice’.
She also costumed Jamie Foxx and Usher Raymond in ‘The Kingdom’, ‘Dream Girls’, ‘Miami Vice’ and ‘In The Mix’.
Richard Nwaobi-E project managed this film and assembled a great cast as the film producer, Dave Boapong, was production manager, with Brian Angels as camera assistant.

 Credit: Francis Addo, NEWS-ONE

Friday, November 25, 2011

POLE SANA SAJUKI TUPO NAWE KATIKA WAKATI HUU MGUMU

    Timu nzima ya Monalisafilms blogspot inaungana na watanzania na wasiokuwa watanzania lakini wanaofahamu fika hali ya kiafya ya msanii wa maigizo Juma Kilowoko al-maarufu kama Sajuki katika kipindi hiki kigumu sana,pamoja tunakuombea upone haraka na kurejea katika shughuli zako za kila siku.
Maombi yetu pia kwa mama Sajuki (Wastara),Mungu akutie nguvu katika kipindi hiki cha kumuuguza mumeo.

Kutoa ni moyo kwa yeyote mwenye chochote kitu kwa nia moja ameamua kumfariji mgonjwa awasiliane na blog hii ya Monalisafilms kwa namba 0718958758 ama email yvonnecherryl@gmail.com na mchango wako utafikishwa mahali husika..

Tuesday, November 22, 2011

MONALISA TO REPRESENT BONGOFILM INTERNATIONALLY

"By the first time i did not expect but time is right here" she said after receiving this......it's simply amazing but she did it.
MONALISA THE BEST ACTRESS IN TANZANIA TO BE FEATURED ALONG SIDE WITH HOLLYWOOD STARS

The best actors and actresses on the African continent have been brought together to feature alongside Hollywood actors in a new movie ‘Bleeding Sunshine’, which is set to hit the theatres soon. The production crew is expected to continue shooting in Egypt, Dubai and Israel.

The ‘Bleeding Sunshine’ movie talks about the “illegal trade of human beings for the purposes of reproductive slavery, commercial sexual exploitation, forced labour, or a modern-day form of slavery” called human trafficking.
The Hollywood feature film brings out a harrowing tale of a young Ghanaian girl [Suzzy Nabor] whose life is turned upside down when she is plucked from her humble fishing village and thrust into the gritty world of international human trafficking.

Tuesday, November 8, 2011

PALE FILAMU ZINAPOTURUDISHA DARASANI

Unaweza kuhisi kwamba pindi unapovaa joho ama la kuhitimu kidato cha nne cha sita ama joho la heshima la chuo kikuu kwamba umemaliza kila kitu kuhusu kusoma dah!!! katika tasnia ya filamu mambo yanarejea kulekule kusoma kama kawaida. halafu mbaya zaidi ukiwa muhusika mkuu kuna kitu kinaitwa SCRIPT wanaoifahamu lugha vizuri wanasema ni mswada,mh!! yaani hapo ni zaidi ya darasa,kama ulikuwa hauna mazoea ya kukaririri 'what is biology,what is civics' sasa huku hakuna ujanja lazima ukaririri kwanza ndo uende mbele ya kamera,halafu huku hakuna cha kuangalizia ukithubutu kuangalizia kamera inakuumbua kwa hiyo lazima ukariri,aliyekwambia unaweza kuielewa script nani??? labda kama hiyo filamu umetunga mwenyewe kichwani,asikwambie mtu jamani script haina cha mzoefu

Hapa kama script inamzingua vile Monalisa,lakini sasa atafanyaje na ndo hiyo ajira yake na huyu mama yangu naye anaandaa hapo script kazi kwenye kukariri halafu mkononi ana pesa dah! sijui mchaga.

Friday, November 4, 2011

MONALISA NA KANUMBA WAINUSA HOLLYWOOD


Dah!! kama utani vile mwanadada mashuhuri katika tasnia ya filamu hapa bongo ambaye anatamba mkononi na tuzo yake ya msanii bora wa kike mwaka jana Yvonne Cherryl ali maarufu kama Monalisa pamoja na pacha wake katika tuzo kwa upande wa wanaume Stevene Kanumba,juhudi zao katika sanaa zinazidi kuzaa matunda huku wakipasua anga zaidi kimataifa na sasa wapo nchi iliyojaa vipaji vya sanaa ya maigizo Ghana. Hawajaenda kula bata kama wengi wanavyodhani bali wameenda kikazi zaidi huku wakiiwakilisha vyema afrika mashariki miongoni mwa vichwa vingine kutoka nchi mbalimbali tayari kwa kupakua mzigo wa maana.

Tuesday, November 1, 2011

MONALISA ABADILI DINI

Hiyo heading huenda imekushtua sana....... hapana usishtuke mbona kawaida kwani wangapi wamebadili dini na bado wanapeta??? kwani dhambi jamani. Hapana jamani alikuwa anatania tu,mwanadada mashuhuri ambaye anakaribia kuitwa nguli katika tasnia ya filamu bongo Yvonne Cherry yupo mzigoni na muda wowote kuanzia sasa msubiri hapo nyumbani kwako katika mzigo mpya anaoupiga na mtaalamu mwenzake Lucie Komba. Jina la picha naweka kapuni lakini mwanadada Monalisa hapo kati akiitwa Salma binti Sudi amevaa uhusika wa kiislamu na kubutua hiyo filamu ambayo bila shaka hajaharibu kitu chochote kama kawaida.
unaweza ukaamini yeye ndo kamvisha hili hijabu mwanadada binti wa Komba najua huwezi kuamini mtazame hapa chini.


hii ilikuwa siku ya kwanza....kwa behind the scene nyingine endelea kufatilia blog hii hadi mwisho wa mchezo

Monday, October 31, 2011

TUWE SAUTI YAO



Naamini hawawezi kusikika hata wakizipaza sauti zao juu sana,si tu kwa sababu sauti zao ziko chini HAPANA ila watanzania wameziba masikio yao wasiweze kuwasikia na kuwasaidia.
Hebu kuwa wa kwanza kufungua masikio yako na kumsikikliza bibi huyu akilia kwa uchungu mkali analia kilio cha upendo,upendo wake unasababisha chozi lake limdondoke. Hana uwezo mkubwa sana lakini ana upendo,kipato chake ni duni lakini bado anahitaji kusaidia wengine,kubwa zaidi ni MLEMAVU lakini hilo halimkatishi tamaa,kutana na bibi huyu katika show malidhawa itakayokujia hivi karibuni
. Je unaamini kwamba waweza kuwa mlemavu lakini bado ukawasaidia wengine wasiojiweza zaidi yako??

"mabadiliko huanzia kwa mmoja na hatimaye dunia nzima" anaonekana akisema mama huyu mlemavu ambaye ana jukumu linalomzidi uzito....vuta subira utamfahamu kiundani hivi karibuni.......

Thursday, October 20, 2011

MONALISA KUISHANGAZA TANZANIA NA DUNIA!!!

Msanii maarufu wa filamu hapa nchini anayewika hadi nchi za watu huku akijivunia kuwa muigizaji bora wa kike kipindi flani hivi sasa anakuja kivingine kuikamata Tanzaniana mipaka yake.....unahisi anaandaa filamu mpya bada ya kutamba naBinti Nusa iliyompa tunzo??...au unadhani anaandaa muziki???...mimi na wewe hatufahamu kama ndo ameamua kuacha sanaa ya filamu ili kuishangaza Tanzania au vipi,yeye mwenyewe hakufunguka sana ila alisema kaneno flani hivi nami namnukuu
"coming soooon!!!!!!" hebu tazama hapa akiwa bize nyuma ya camera katika hizo location hapa juzi kati.

hapa mama na mwana...Monalisa akiwa anaandika masuala kadhaa soon baada ya kufika location.

I AM BACK


Ni siku nyingi sana nimekuwa kimya katika ulimwengu huu wa blogu lakini sasa nimerejea mzima mzima kuendelea kuwa nanyi karibu,kuwajuza nanyi kunijulisha mambo kadha wa kadha katika tasnia hii ya filamu zetu za kibongo. Fuatana nami upya tena kama zamani........hebu ngoja niwapigie namba zenu kama mnapatikana maana na nyie kwa kubadili namba siwawezi

Saturday, March 5, 2011

Nimetembelea Kambi ya Yatima na Wazee wasiojiweza na kula lunch pamoja nao


Nungwi-Kigamboni kwenye kambi ya yatima na wazee wasiojiweza zamani ikifahamika kama kambi ya wenye Ukoma ndiko nilipotembelea weekend hii na kula lunch pamoja nao.Chakula kilichopikwa na sisi wenyewe katika kikundi chetu cha wanawake cha Hybiscus



Hapa tukipata msosi na kupiga story mbili tatu na bibi huyu ambaye ni mgonjwa na anayeishi kambini hapo,alifurahi sana.


Chakula bila maji?Nikiwahudumia watoto



Huyu mtoto alinitia majonzi na kunidondosha chozi....Ni yatima na hapo kambini yupo yeye na wadogo zake wawili.Alinipenda sana nami nimempenda sana pia



Akiendelea kunielezea mkasa wake


ITS TIME TO GO,Tukawaachia na zawadi ndogo ya vyakula tulivyojaaliwa kununua.michele,unga,mafuta,sabuni na vitu kama hivyo ili viweze kuwafariji na kufahamu kuwa kuna watu mahala fulani ambao tunaguswa kwa namna moja au nyingine na matatizo yao.

Saturday, February 26, 2011

BONGO MOVIES FC VS BONGO FLAVA FC


Match kati ya Bongo Movies FC na Bongo Flava FC iliyofanyika jana Jumaamosi katika Uwanja mpya wa TAIFA kwa ajili ya kuchangia wenzetu waliokutwa na janga la mabomu ya Gongo la mboto na wengine kupoteza maisha.Hicho ndio Kikosi cha Bongo Movies FC



shitua kama Joti,cheza kama Joti,cheza kijotijoti ha ha ha......Joti wa Original Komedi ndani ya nyumba.


2nd half,hapa Bongo Movies FC tumeshafungwa kwa taabu sana goli 2.Magoli yote ya Bongo Flava FC yakifungwa na H.BABA alituudhi sana na ALI KIBA ndio alifanya sifa kama anataka kusajiliwa na YANGA vile


Wema Sepetu na Jacky Pentezel wakifuatilia Mechi



My mama( Susan Lewis Natasha) na Ephraim Kibonde.......kabla ya mechi kuanza



OH! My best Radio Presenter Millard Ayo huyoooooooooooo


My friend who is also One of Bongo movies show Producers,Felix Awino na Eva Dude



Suda Mwilima wa STAR TV akimhoji Malkia wa mipasho.Top in Town Khadija Omari Kopa


Hapa KOLETHA,MAMA na Mzee CHILLO ambaye alikuwa mmoja wa kamati ya ufundi


Yvonne Cherryl...............




ha ha ha na Jezi yangu na bado tukafungwa

Me,Devotha Mbaga,Mama na Jackline Wolper

For the first time,naweza sema wasanii bongo wamefanya kitu kikubwa sana kwa ajili ya maslahi ya jamii yetu.Ni kitu cha kuwapongeza kwa kweli.

Monday, February 21, 2011

JUKWAA LA SANAA -BASATA


MH.MBUNGE WA MBEYA MJINI KWA TIKETI YA CHADEMA,JOSEPH MBILINYI NAYE ALIKUWEPO KWENYE JUKWAA LA SANAA LINALOFANYIKA KILA SIKU YA J3 KATIKA OFISI ZA BASATA PALE ILALA-DAR ES SALAAM


JUKWAA LA SANAA HUWASHIRIKISHA WADAU MBALIMBALI AMBAO HUTOA MAONI NA PENGINE KUULIZA MASWALI KUHUSIANA NA MADA KUU YA SIKU HIYO.KAMA HAPA MWANAMUZIKI WA MUZIKI WA ASILI CHE MUNDU GWAO AKIULIZA SWALI



KATIBU MTENDAJI WA BASATA GONCHE MATEREGO AKIHITIMISHA MADA NA KUFUNGA MDAHALO WA SIKU HIYO PEMBENI NI PROFESSOR AMANDINA LIHAMBA ALIYEKUWA MWENYEKITI WA MDAHALO HUO



MADA KUU WA SIKU HIYO NI HISTORIA YA FILAMU,CHANGAMOTO NA MAFANIKIO YAKE.HAPA MH.SUGU KAMA TULIVYOZOEA KUMUITA AKISISITIZA JAMBO

KWAKUWA MADA ILIKUWA NI HISTORIA YA FILAMU.....TULIALIKWA MIMI(YVONNE cHERRYL),SINGLE MTAMBALIKE(RICH RICH) NA DOKTA MONA MWAKALINGA TOKA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM KUWA WAONGEAJI WAKUU WA MADA HII.
TUNAWAPONGEZA BASATA KWA KUWA NA JUKWAA HILI KILA WIKI,LINASAIDIA SANA KATIKA KUONGELEA MASUALA MBALIMBALI YAHUSUYO SANAA TANZANIA.