Tuesday, November 10, 2015

Daddy's Wedding Trailer

One of the Best Movies ever made in Tanzania, by Tanzanians so far....congratulations to the Director, Honeymoon Aljabri for a wonderful Job. you really deserve more awards and appreciations for the efforts that you made on it. Proudly Tanzanians.
Daddy's Wedding.
Watch a trailer here!
Moja ya filamu Bora tanzania zilizowahi kutengenezwa nchini Tanzania mpaka sasa. Pongezi kwa Muongozaji, Honeymoon Aljabri kwa kazi nzuri uliyoifanya. filamu halisi ya Kitanzania.
Daddy's Wedding.
Angalia Trailer hapa.

Monday, February 13, 2012

MSIBA WA MZEE KIPARA

 MIMI NA LUCY KOMBA TUKIINGIA MSIBANI MAENEO YA KIGOGO KWENYE NYUMBA YA KAOLE SANAA GROUP  AMBAPO MAREHEMU ALIKUWA AKIISHI HAPO HADI UMAUTI ULIPOMFIKA TAREHE 11/1/2012
 SUSAN LEWIS NATASHA NA WAKINAMAMA MSIBANI


MH.SITTA NA MZEE MAPILI PAMOJA NA WAOMBOLEZAJI WAKIMUAGA MZEE KIPARA


KANUMBA NA WAKINA BABA WAKIMSINDIKIZA MZEE WETU KIPARA KWENYE NYUMBA YAKE YA MILELE

 HERIETH CHUMIRA,ME,LUCY KOMBA NA SOUD ALLY

DEVOTHA MBAGA ,NORA,MAYA NA WENGINEO WALIKUWEPO PIA MSIBANI
SISI TULIMPENDA FUNDI SAID ALMAARUFU MZEE KIPARA,LAKINI MUNGU AMEMPENDA ZAIDI.

Tuesday, February 7, 2012

MINI ZIFF RED CARPET

 Red Carpet ya Mini Ziff
Location: Maisha Club,Oyster bay.

Swahiba Steven Kanumba alipata Tuzo mbili ya msanii bora wa kiume na The Best Sound...Filamu ya Devil Kingdom aliyofanya na Ramsey Tokumbo Noah wa Nigeria.Big Up Dogo

 Aunty Ezekiel na Dennis Sweya aka Dino ndani


 Baby Madaha naye ndani ya Red Carpet bila kukosa anatamba na Muvi yake mpya hivi sasa ya RAY OF HOPE iliyoshinda Tuzo ya Filamu bora kwa mujibu wa ZIff ya Mwaka jana


Mambo hayo ya zamani hapo....Single Mtambalike,me na my Sweet mama....Inapendeza

 
Hisani Muya aka Tino,me and Dino
 MINI ZIFF ilitoa tuzo kwa watu na Makampuni 10 waliyofanya vizuri kwa 2011
BEST DIRECTOR-ISSA MUSA CLOUD
BEST SOUND-DEVIL KINGDOM(KANUMBA)
BEST MOVIE-SENIOR BACHELOR(JB)
BEST UPCOMING-JUMA(ZOBA)
BEST DISTRIBUTOR-PILIPILI AND,STEPS ENTERTAINMENT
HONORARY AWARD-THECKLA MJATA
THE MOST INFLUENCIAL ICON-VINCENT KIGOSI(RAY)
BEST ACTOR-STEVEN KANUMBA
BEST ACTRESS-ROSE NDAUKA
Tuesday, January 10, 2012

filming ya Trailer ya BLEEDING SUNSHINE.. ACCRA,GHANABLEEDING SUNSHINE Filamu ya kiafrika itakayoshirikisha mastaa wa Hollywood,hapa tulikuwa tunashoot trailer yake huko Accra,kwa akina Majid Michel,John Dumelo,Nadia Buari,Jacki Appiah na mastaa kibao wa nchi hiyo.


D.O.P,Director of photography wa filamu hiyo kutoka Hollywood,CHASE BOWMAN na 2nd Asst.DOP wake wakiwa mzigoni
Ha ha ha Tigo jamani Tigo kah!na yenyewe inataka kuuza suraHiyo scene ilikuwa ya shule,usishangae kuona wanafunzi wengi.ni kushangaa tu!nani amekuambia Buguruni tu ndio watu wanashangaa Hata kwao hivyo hivyo ha ha ha


Hao ni mastaa wa Ghana waliokuwa wakicheza kama wanafunzi katika Scene hiyo.Yule pembeni mama mjamzito ndiyo mtayarishaji na muongozaji wa filamu hiyo.Mzaliwa wa Ghana,Raia wa Marekani anayefanya kazi huko Hollywood anaitwa Yaa Boa Anning.
Nilienjoy sana kipindi chote cha Production hiyo na kujifunza vitu vingi vipya lakini kikubwa pia kujifunza lugha tofauti za nchi hiyo lakini neno rahisi ambalo hata wewe utalishika kirahisi sema AKWAABA.....linamaanisha KARIBU.Imetulia eh?

Sunday, January 1, 2012

BONGO MOVIES BEACH PARTY 2011


from right:Jack wolper,Ummy aka Dokii,na mimi mwenyewe

Kila mwisho wa mwaka,kampuni ya usambazaji wa Filamu nchini STEPS hufanya beach party ya kufunga mwaka na kuwashukuru wasanii na watayarishaji wa filamu ambao wamefanya nao kazi.
 Jacob Stephen ambaye tumetoka naye mbali sana tangu enzi za mambo hayo,unakumbuka?naye bila kukosa.

 Susan Lewis aka Natasha aka Mama yangu,ha ha ha hiyo ya pili sio aka bwana.....mama yangu kipenzi naye apitwe?

 From left:Jenifa Kyaka aka Odama,Me,na Mayasa Mrisho aka Maya

 Mkurugenzi wa Steps Entertainment Ltd Mr.Dilesh akinikabidhi Certificate of Appreciation iliyosomeka THERE'S NO S-CCES WITHOUT U!Imetulia

 Tukipiga story kidogo na bibie Salama Salmin aka Sandra huku vikuku vikipanda kwa mbali,umekosaje?

Mwisho mzee wa Relax akinipa shavu,ha ha ha Peter Msechu naye aliyekuwepo

Party ilifanyika Sunrise Beach Hotel Kigamboni.Ilikuwa Party nzuri kwakweli,Inafrica Band ilikuwepo na vikundi mbalilmbali kuachilia mbali watayarishaji wote wa filamu Tanzania unaowafahamu.

Monday, December 26, 2011

MIAKA 20 KATIKA GAME BILA KUCHUJA,LUNDO LA TUNZO!!!

Ana miongo miwili katika tasnia ya filamu hapa nchini akiwa amepiga hatua hadi nje ya Tanzania, mbali zaidi ameusogeza mguu wake mmoja katika dreamland ya wa sanii wengi,"kuingia Hollywood".
Ameianza tasnia hii tangu akiitwa mtoto, baadaye msichana halafu hadi sasa anapoitwa mzazi bado anapeta katika game hili.
Kampuni inayozalisha magazeti pendwa ya burudani hapa yaani Global publishers nchini ililithibitisha hili kwa umma baada ya kufanya shindano baab kubwa lililowapambanisha wakali mbalimbali katka fani mbalimbali za saana hapa nchini, ni kura ya msomaji ilikuwa inaamua mshindi ni nani.
HAPA AKIWA MZIGONI si unajua kwama ana taaluma ya kuongoza filamu!!!!!!
HALAFU HAPA AKIWA MAMA......na mtoto wake wa mwisho kwa sasa
Kama kura zilipigwa na msomaji basi mwanadada Yvonne Cherryl Monalisa anakubalika ile sana, amefunika mastaa wote wa kike ambao ni maarufu na kuingia katika kumi bora ya kuwania tuzo zinazotolewa na kampuni hiyo ya Global Publishers zinazokwenda kwa jina la Tanzania Walk Of Fame. Katika orodha hiyo wanaume ni wanne na Monalisa akiungana na Jaydee,Bi. Kidude, na Rose Mhando katika kundi la wanawake wanne wa shoka hapa Bongo linapokuja suala la kuitunza Nyota ya umaarufu.

Thursday, December 22, 2011

POLENI KWA MAFURIKO TANZANIA

Ni jambo la kusikitisha sana lakini yote ni mipango ya Mungu huu si wakati muafaka wa kuwalaumu waliojenga mabondeni licha ya kupewa maonyo mara kwa mara bali ni wakati wa kuangalia nini tunafanya

hizi ni baadhi ya sehemu.......unaweza kuamini hapa ni barabarani???? yeah!! kama we ni wa hapa Dar na ulikuwa katika mizunguko ya hapa na pale siku ya jana na juzi waweza kuwa shahidi.
 kama utani vilelakini huu ndio ukweli ilivyokuwa jana hapa jijini.......wamepoteza makazi hao tayari,serikali!!!!!!!! wapiga kura wenu hao,lakini na wewe mtanzania jirani yako huyo