Saturday, November 26, 2011

PIC OF THE WEEK

Kalsoume Sinare and I,Accra-Ghana.March,2011

Kalsoume Sinare,ni mmoja kati ya waigizaji wakongwe na mahiri wa Ghallywood.Yeye ndiye alikuwa symbol yangu kwa miaka ya nyuma katika kufahamu kwamba hii ni filamu ya ghana.Amekuwepo kwa muda mrefu sana,tangu alikuwa akicheza kama kasichana,na sasa bado anaendelea kukimbiza tu.

Mara yangu ya kwaza kabisa kutia maguu Accra,yeye ndiye mtu wa kwanza nilliyekuwa nawish kummeet na kubadilishana naye mawazo mawili matatu kuhusiana na kiwanda cha filamu sio Bongo wala cha Ghana,bali kiwanda cha filamu Africa.Ni ndoto yangu kuona siku moja Producer wa Nollwood anapoandaa filamu anaanza kufikiria Cast kutoka Angola,au Rwanda.Producer wa Bongo anamfikiria msanii wa Ghana au South Africa,Producer wa Ghana anamfikiria msanii wa Kibongo au Burundi,INAWEZEKANA.

I was so excited kukutana na Kalsoume Japo kwa bahati mbaya hakuwa wa kwanza tena kukutana naye kama ilikvyokuwa ndoto yangu kwani nilishakutana na MAJID MICHEL, na ADJETEY ANANG.Lakini Kalsoume alinipokea vizuri sana,ni mcheshi na mkarimu.Nilienjoy kwa kweli,na akaniinvite dinner mara nyingine nitakayokuwa huko,japo niliporudi tena in Sept..i was so busy na mambo mengine hatukuonana.

Kalsoume ni mke na mama wa watoto wawili wa Kiume.

1 comment:

  1. mependendeza na mefurahi pia kumjua Kalsoume wa Ghana , big up kwa hili na mungu akutangulie katika kazi zako.

    ReplyDelete