Monday, February 13, 2012

MSIBA WA MZEE KIPARA

 MIMI NA LUCY KOMBA TUKIINGIA MSIBANI MAENEO YA KIGOGO KWENYE NYUMBA YA KAOLE SANAA GROUP  AMBAPO MAREHEMU ALIKUWA AKIISHI HAPO HADI UMAUTI ULIPOMFIKA TAREHE 11/1/2012
 SUSAN LEWIS NATASHA NA WAKINAMAMA MSIBANI


MH.SITTA NA MZEE MAPILI PAMOJA NA WAOMBOLEZAJI WAKIMUAGA MZEE KIPARA


KANUMBA NA WAKINA BABA WAKIMSINDIKIZA MZEE WETU KIPARA KWENYE NYUMBA YAKE YA MILELE

 HERIETH CHUMIRA,ME,LUCY KOMBA NA SOUD ALLY

DEVOTHA MBAGA ,NORA,MAYA NA WENGINEO WALIKUWEPO PIA MSIBANI
SISI TULIMPENDA FUNDI SAID ALMAARUFU MZEE KIPARA,LAKINI MUNGU AMEMPENDA ZAIDI.

Tuesday, February 7, 2012

MINI ZIFF RED CARPET

 Red Carpet ya Mini Ziff
Location: Maisha Club,Oyster bay.

Swahiba Steven Kanumba alipata Tuzo mbili ya msanii bora wa kiume na The Best Sound...Filamu ya Devil Kingdom aliyofanya na Ramsey Tokumbo Noah wa Nigeria.Big Up Dogo

 Aunty Ezekiel na Dennis Sweya aka Dino ndani


 Baby Madaha naye ndani ya Red Carpet bila kukosa anatamba na Muvi yake mpya hivi sasa ya RAY OF HOPE iliyoshinda Tuzo ya Filamu bora kwa mujibu wa ZIff ya Mwaka jana


Mambo hayo ya zamani hapo....Single Mtambalike,me na my Sweet mama....Inapendeza

 
Hisani Muya aka Tino,me and Dino
 MINI ZIFF ilitoa tuzo kwa watu na Makampuni 10 waliyofanya vizuri kwa 2011
BEST DIRECTOR-ISSA MUSA CLOUD
BEST SOUND-DEVIL KINGDOM(KANUMBA)
BEST MOVIE-SENIOR BACHELOR(JB)
BEST UPCOMING-JUMA(ZOBA)
BEST DISTRIBUTOR-PILIPILI AND,STEPS ENTERTAINMENT
HONORARY AWARD-THECKLA MJATA
THE MOST INFLUENCIAL ICON-VINCENT KIGOSI(RAY)
BEST ACTOR-STEVEN KANUMBA
BEST ACTRESS-ROSE NDAUKA




Tuesday, January 10, 2012

filming ya Trailer ya BLEEDING SUNSHINE.. ACCRA,GHANA



BLEEDING SUNSHINE Filamu ya kiafrika itakayoshirikisha mastaa wa Hollywood,hapa tulikuwa tunashoot trailer yake huko Accra,kwa akina Majid Michel,John Dumelo,Nadia Buari,Jacki Appiah na mastaa kibao wa nchi hiyo.






D.O.P,Director of photography wa filamu hiyo kutoka Hollywood,CHASE BOWMAN na 2nd Asst.DOP wake wakiwa mzigoni




Ha ha ha Tigo jamani Tigo kah!na yenyewe inataka kuuza sura



Hiyo scene ilikuwa ya shule,usishangae kuona wanafunzi wengi.ni kushangaa tu!nani amekuambia Buguruni tu ndio watu wanashangaa Hata kwao hivyo hivyo ha ha ha


Hao ni mastaa wa Ghana waliokuwa wakicheza kama wanafunzi katika Scene hiyo.Yule pembeni mama mjamzito ndiyo mtayarishaji na muongozaji wa filamu hiyo.Mzaliwa wa Ghana,Raia wa Marekani anayefanya kazi huko Hollywood anaitwa Yaa Boa Anning.
Nilienjoy sana kipindi chote cha Production hiyo na kujifunza vitu vingi vipya lakini kikubwa pia kujifunza lugha tofauti za nchi hiyo lakini neno rahisi ambalo hata wewe utalishika kirahisi sema AKWAABA.....linamaanisha KARIBU.Imetulia eh?

Sunday, January 1, 2012

BONGO MOVIES BEACH PARTY 2011


from right:Jack wolper,Ummy aka Dokii,na mimi mwenyewe

Kila mwisho wa mwaka,kampuni ya usambazaji wa Filamu nchini STEPS hufanya beach party ya kufunga mwaka na kuwashukuru wasanii na watayarishaji wa filamu ambao wamefanya nao kazi.
 Jacob Stephen ambaye tumetoka naye mbali sana tangu enzi za mambo hayo,unakumbuka?naye bila kukosa.

 Susan Lewis aka Natasha aka Mama yangu,ha ha ha hiyo ya pili sio aka bwana.....mama yangu kipenzi naye apitwe?

 From left:Jenifa Kyaka aka Odama,Me,na Mayasa Mrisho aka Maya

 Mkurugenzi wa Steps Entertainment Ltd Mr.Dilesh akinikabidhi Certificate of Appreciation iliyosomeka THERE'S NO S-CCES WITHOUT U!Imetulia

 Tukipiga story kidogo na bibie Salama Salmin aka Sandra huku vikuku vikipanda kwa mbali,umekosaje?

Mwisho mzee wa Relax akinipa shavu,ha ha ha Peter Msechu naye aliyekuwepo

Party ilifanyika Sunrise Beach Hotel Kigamboni.Ilikuwa Party nzuri kwakweli,Inafrica Band ilikuwepo na vikundi mbalilmbali kuachilia mbali watayarishaji wote wa filamu Tanzania unaowafahamu.