NB: Mada hii imejadiliwa na wapenzi wa filamu katika ukurasa
wa facebook....monalisafilms. maoni hayo si kutoka blog hii
moja kwa moja.
Soko la
filamu bongo linazidi kutanuka kila kukicha japo bado zinahitajika hatua nyingi
mbele kufikia viwango vya kimataifa kama ilivyo kwa nchi za naijeria,Ghana na
hata jirani zetu wa Kenya.
Tanzania
ikiwa imejikita katika tasnia ya filamu tangu mwanzoni mwa mwaka 2000 hadi sasa
ni zaidi ya filamu 500 tofautitofuti zimekwishayafikia macho ya wapenzi wa
filamu,kila mlaji (mnunuzi) wa filamu amekuwa akivutiwa na muigizaji wake ama
mudhui ya filamu Fulani,mfano wapo wanaovutiwa na sinema za kivita,wengine
mapenzi na wengine vichekesho.
Je wasanii
wetu wanakidhi haja ya mlaji wao?? Hilo ndilo swali lililozuka na kuzua hii
mada. Wachangiaji wakuu wakiwa ni wafuatiliaji wa filamu za hapa kwetu.
Majibu yalikuw
tofautitofauti lakini malalamiko makubwa yalikuwa kwamba filamu nyingi za sasa
katika soko zinjirudiarudia ama ni za kuiga kutoka nchi za wenzetu na kubadili
lugha tu….na hapo ndipo swali la pili ambalo linaiendesha hii mada likiibuka,kwamba
nani alaumiwe kwa hizi filamu kujirudia rudia???
"SAADIZM"
UFINYU WA MAWAZO YA WATUNZI: Watunzi wengi kwa sasa wanakosa
ubunifu,mtunzi akiwa dereva mkuu wa filamu inayokufikia nyumbani kwako anakuwa
mvivu wa kutunga kitu cha kipekee na badala yake anaiga kutoka nje stori ileile
na kuibadilisha lugha kisha kwa ujasiri anaifikisha kwa mtanzania kama filamu
mpya.
"KALUONA KINAWILO"
ELIMU YA SANAA:Waandaaji,wasimamizi na hata
waigizaji wana kiwango kidogo cha elimu ya sanaa,wengi wao wamevamia fani kwa
malengo tofauti hasahasa kutafuta umaarufu mtaani jambo hili linawalazimu
kuchukua muda mrefu kupitia filamu za watu na kuchota kidogo kidogo ili na wao
wafanye filamu hii inaturudisha katika giza ambalo tulikuwa tunaliacha.
"MICHAEL MSOMBE"
MIKATABA MIGUMU: kuna baadhi ya wasambazaji wana
masharti magumu kwa wateja wao,utakuta mwandaaji amemsainisha mkataba mteja
wake (msanii) unaomtaka kutoa filamu moja hadi mbili kwa mwezi yaani kwa mwaka
filamu 24 za msanii mmoja ziingie sokoni,hapa kitatokea nini kama si
kujirudiarudia kwa ujumbe kasoro wahusika?? Kwa hali halisi haiwezekani kichwa
kimoja kitunge filamu 24 zote zikiwa na utofauti.
"JOEL RENATUS"
MWANDISHI WA SCRIPT: Mazoea ya kumtumia mwandishi mmoja
wa script katika filamu sio tu kwamba inadidimiza ama kuu vipaji vya waandishi
wengine ila ni chanzo pia cha filamu kuwa na ujumbe unaofanana,mfano halisi ni
katika utunzi wa vitabu vya simulizi,ladha ya kitabu cha Beka Mfaume ni tofauti
na ile ya marehemu Ben Mtobwa. Na kama ni msomaji mzuri wa vitabu hata kama
hujasoma gamba la nje la kitabu utagundua mwandishi ni nani. Hivyo haya mazoea
yanaathiri sana filamu zetu.
"
PESA MBELE UBORA BAADAYE: wasanii wengi sasa wameweka pesa mbele
huku wakimdharau mtanzania ambaye amekubali kuwa mtumwa wa kazi zao. Hawajali kuwa
filamu ni mbovu ama inalandana na filamu ya fulani wanachoangalia ni mifukoni
itaingia shilingi ngapi,hivyo hivyo kwa msambazaji ananunua filamu bila
kuchukua wakati kuzipitia walau kidogo,matokeo yake anasambaza filamu ambayo
miezi miwili iliyopita alisambaza pia.
"HAILLE SELLASIE"
UDHAIFU WA BODI YA FILAMU: Bodi ya filamu Tanzania ni kama haipo vile,hiki
ndicho chombo kikuu chenye madaraka ya kuuondoa huu uozo,lakini wamekuwa kimya
sana na filamu zinaendelea kupeta licha ya kufanana fanana. Laiti kama filamu
kadhaa zingefungiwa nadhani wengine wangeshtuka na kubadilika….mzani wa kupim
filamu UNAHITAJIKA!!!!
"BEATRICE NYOROKA"
KUJILIMBIKIZIA MADARAKA: mwanzoni wakati msanii anaanza
kuibukia unakuta anajitambulisha kama muigizaji lakini baada ya kupata jina
kidogo tu utasikia oooh!! Mi mtunzi wa stori,mara naandika script kabla
hatujakaa sawa mara anasema yeye director na pia ana idea ya kuedit hivyo muda
si mrefu ataanza kuedit movie zake. Kwa mtindo huo wa kujifanya kujua kila kitu
kweli atakawia kuiba filamu za nje na kutubadilishia lugha???.
"BOAZ KIM"
NATAKA KUWA KANUMBA: Katika mpira wa miguu ukimuuliza
chipukizi ana ndoto gani atakujibu anataka kucheza ulaya lakini ukimuuliza
msanii mchanga wa bongo ndoto yake ni ipi katika hii tasnia atakujibu “nataka
kuwa kama kanumba” kwa ndoto hii sasa atajaribu kuigiza kama Kanumba na mwisho
wa siku atatunga stori anazotunga Kanumba na hatimaye atatoa filamu kama ya
Kanumba,sijui hapo ndo kutimiza ndoto ama kulivuruga soko la filamu. Si kwamba watu
wasiwe na ndoto lakini zisiwe ndoto za kufananisha kazi.
No comments:
Post a Comment