Monday, December 26, 2011

MIAKA 20 KATIKA GAME BILA KUCHUJA,LUNDO LA TUNZO!!!

Ana miongo miwili katika tasnia ya filamu hapa nchini akiwa amepiga hatua hadi nje ya Tanzania, mbali zaidi ameusogeza mguu wake mmoja katika dreamland ya wa sanii wengi,"kuingia Hollywood".
Ameianza tasnia hii tangu akiitwa mtoto, baadaye msichana halafu hadi sasa anapoitwa mzazi bado anapeta katika game hili.
Kampuni inayozalisha magazeti pendwa ya burudani hapa yaani Global publishers nchini ililithibitisha hili kwa umma baada ya kufanya shindano baab kubwa lililowapambanisha wakali mbalimbali katka fani mbalimbali za saana hapa nchini, ni kura ya msomaji ilikuwa inaamua mshindi ni nani.
HAPA AKIWA MZIGONI si unajua kwama ana taaluma ya kuongoza filamu!!!!!!
HALAFU HAPA AKIWA MAMA......na mtoto wake wa mwisho kwa sasa
Kama kura zilipigwa na msomaji basi mwanadada Yvonne Cherryl Monalisa anakubalika ile sana, amefunika mastaa wote wa kike ambao ni maarufu na kuingia katika kumi bora ya kuwania tuzo zinazotolewa na kampuni hiyo ya Global Publishers zinazokwenda kwa jina la Tanzania Walk Of Fame. Katika orodha hiyo wanaume ni wanne na Monalisa akiungana na Jaydee,Bi. Kidude, na Rose Mhando katika kundi la wanawake wanne wa shoka hapa Bongo linapokuja suala la kuitunza Nyota ya umaarufu.

No comments:

Post a Comment