Monday, October 31, 2011

TUWE SAUTI YAO



Naamini hawawezi kusikika hata wakizipaza sauti zao juu sana,si tu kwa sababu sauti zao ziko chini HAPANA ila watanzania wameziba masikio yao wasiweze kuwasikia na kuwasaidia.
Hebu kuwa wa kwanza kufungua masikio yako na kumsikikliza bibi huyu akilia kwa uchungu mkali analia kilio cha upendo,upendo wake unasababisha chozi lake limdondoke. Hana uwezo mkubwa sana lakini ana upendo,kipato chake ni duni lakini bado anahitaji kusaidia wengine,kubwa zaidi ni MLEMAVU lakini hilo halimkatishi tamaa,kutana na bibi huyu katika show malidhawa itakayokujia hivi karibuni
. Je unaamini kwamba waweza kuwa mlemavu lakini bado ukawasaidia wengine wasiojiweza zaidi yako??

"mabadiliko huanzia kwa mmoja na hatimaye dunia nzima" anaonekana akisema mama huyu mlemavu ambaye ana jukumu linalomzidi uzito....vuta subira utamfahamu kiundani hivi karibuni.......

No comments:

Post a Comment