Saturday, March 5, 2011

Nimetembelea Kambi ya Yatima na Wazee wasiojiweza na kula lunch pamoja nao


Nungwi-Kigamboni kwenye kambi ya yatima na wazee wasiojiweza zamani ikifahamika kama kambi ya wenye Ukoma ndiko nilipotembelea weekend hii na kula lunch pamoja nao.Chakula kilichopikwa na sisi wenyewe katika kikundi chetu cha wanawake cha Hybiscus



Hapa tukipata msosi na kupiga story mbili tatu na bibi huyu ambaye ni mgonjwa na anayeishi kambini hapo,alifurahi sana.


Chakula bila maji?Nikiwahudumia watoto



Huyu mtoto alinitia majonzi na kunidondosha chozi....Ni yatima na hapo kambini yupo yeye na wadogo zake wawili.Alinipenda sana nami nimempenda sana pia



Akiendelea kunielezea mkasa wake


ITS TIME TO GO,Tukawaachia na zawadi ndogo ya vyakula tulivyojaaliwa kununua.michele,unga,mafuta,sabuni na vitu kama hivyo ili viweze kuwafariji na kufahamu kuwa kuna watu mahala fulani ambao tunaguswa kwa namna moja au nyingine na matatizo yao.

Saturday, February 26, 2011

BONGO MOVIES FC VS BONGO FLAVA FC


Match kati ya Bongo Movies FC na Bongo Flava FC iliyofanyika jana Jumaamosi katika Uwanja mpya wa TAIFA kwa ajili ya kuchangia wenzetu waliokutwa na janga la mabomu ya Gongo la mboto na wengine kupoteza maisha.Hicho ndio Kikosi cha Bongo Movies FC



shitua kama Joti,cheza kama Joti,cheza kijotijoti ha ha ha......Joti wa Original Komedi ndani ya nyumba.


2nd half,hapa Bongo Movies FC tumeshafungwa kwa taabu sana goli 2.Magoli yote ya Bongo Flava FC yakifungwa na H.BABA alituudhi sana na ALI KIBA ndio alifanya sifa kama anataka kusajiliwa na YANGA vile


Wema Sepetu na Jacky Pentezel wakifuatilia Mechi



My mama( Susan Lewis Natasha) na Ephraim Kibonde.......kabla ya mechi kuanza



OH! My best Radio Presenter Millard Ayo huyoooooooooooo


My friend who is also One of Bongo movies show Producers,Felix Awino na Eva Dude



Suda Mwilima wa STAR TV akimhoji Malkia wa mipasho.Top in Town Khadija Omari Kopa


Hapa KOLETHA,MAMA na Mzee CHILLO ambaye alikuwa mmoja wa kamati ya ufundi


Yvonne Cherryl...............




ha ha ha na Jezi yangu na bado tukafungwa

Me,Devotha Mbaga,Mama na Jackline Wolper

For the first time,naweza sema wasanii bongo wamefanya kitu kikubwa sana kwa ajili ya maslahi ya jamii yetu.Ni kitu cha kuwapongeza kwa kweli.

Monday, February 21, 2011

JUKWAA LA SANAA -BASATA


MH.MBUNGE WA MBEYA MJINI KWA TIKETI YA CHADEMA,JOSEPH MBILINYI NAYE ALIKUWEPO KWENYE JUKWAA LA SANAA LINALOFANYIKA KILA SIKU YA J3 KATIKA OFISI ZA BASATA PALE ILALA-DAR ES SALAAM


JUKWAA LA SANAA HUWASHIRIKISHA WADAU MBALIMBALI AMBAO HUTOA MAONI NA PENGINE KUULIZA MASWALI KUHUSIANA NA MADA KUU YA SIKU HIYO.KAMA HAPA MWANAMUZIKI WA MUZIKI WA ASILI CHE MUNDU GWAO AKIULIZA SWALI



KATIBU MTENDAJI WA BASATA GONCHE MATEREGO AKIHITIMISHA MADA NA KUFUNGA MDAHALO WA SIKU HIYO PEMBENI NI PROFESSOR AMANDINA LIHAMBA ALIYEKUWA MWENYEKITI WA MDAHALO HUO



MADA KUU WA SIKU HIYO NI HISTORIA YA FILAMU,CHANGAMOTO NA MAFANIKIO YAKE.HAPA MH.SUGU KAMA TULIVYOZOEA KUMUITA AKISISITIZA JAMBO

KWAKUWA MADA ILIKUWA NI HISTORIA YA FILAMU.....TULIALIKWA MIMI(YVONNE cHERRYL),SINGLE MTAMBALIKE(RICH RICH) NA DOKTA MONA MWAKALINGA TOKA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM KUWA WAONGEAJI WAKUU WA MADA HII.
TUNAWAPONGEZA BASATA KWA KUWA NA JUKWAA HILI KILA WIKI,LINASAIDIA SANA KATIKA KUONGELEA MASUALA MBALIMBALI YAHUSUYO SANAA TANZANIA.

Sunday, February 13, 2011

Monalisa kuhost Bongo Movies Show


Yvonne cherryl Monalisa aka malkia wa Bongo movies ataanza kuonekana jumaatano hii ndani ya EastAfrica Television kwenye kipindi cha Bongo movies.
Kipindi hicho huzungumzia masuala yote yanayohusiana na tasnia ya filamu Tanzania.

Joyce Kiria aliyekuwa stering wa kipindi cha Bongo Movies kwa muda mrefu ambaye pia ni mtayarishaji wa kipindi hicho akiwa na Yvonne Cherryl kabla ya kuanza kurekodi kipindi




Jumaatano hii na zingine zinazofuata usikose kuangalia show hiyo saa tatu na nusu usiku,EATV na Yvonne Cherryl

Sunday, January 16, 2011

AHSANTE FILAMU CENTRAL

FILAMUCENTRAL YAZAWADIA WASHINDI WA BORA ZA 2010 TAR.14 JAN,TAMAL HOTEL,MWENGE. MTAYARISHAJI WA THE AMPLIFIER YA MILLARD AYO,CLOUDS FM AKINIHOJI KUHUSIANA NA TUZO HIYO NILIYOSHINDA YA MSANII BORA WA KIKE 2010


DOGO JENIFER,MSANII BORA CHIPUKIZI.STEVEN KANUMBA-MSANII BORA WA KIUME,YVONNE CHERRYL-MSANII BORA WA KIKE,ALLY YAKUTI-MWANDISHI BORA WA MUSWADA(SCRIPT) NA MWALUBADU-MCHEKESHAJI BORA


NIKIFURAHIA JAMBO


SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWA MASHABIKI WANGU WALIONIPIGIA KURA NA HATA WALE AMBAO HAWAKUPATA NAFASI YA KUFANYA HIVYO KWANI NAJUA TUPO PAMOJA NA WANAFURAHIA USHINDI HUU PAMOJA NAMI.....NITAENDELEA KUWAAMBIA NAWAPENDA SANA KILA SIKU MNAENDELEA KUNIPA HESHIMA...AHSANTENI SANA

AHSANTE MAMA(SUSAN LEWIS-NATASHA)KWA KUNISHONEA NGUO NZURI ILIYONIFANYA NIPENDEZE,NAKUPENDA MAMA YANGU NA UNALIJUA HILO.MUNGU AKUZIDISHIE.

Thursday, December 30, 2010

no.2 TUKIO LILILONIFURAHISHA.....CHERRIE CO.LTD

Namshukuru sana Mungu,kwa kuniwezesha kusimama tena na kufungua kampuni yangu inayojihusisha na mambo ya filamu. Kuanzia 2011,wadau wangu kaeni tayari kupokea vitu vizuri toka CHERRIE CO.LTD kwa kuanzia tumeanza na BINTI NUSA ambayo pia tumeisambaza wenyewe. Kwangu si mara ya kwanza kuwa na kampuni,japo kuna ups and downs zilizojitokeza.lakini hii najivunia nayo zaidi,Kwani nimekuja kivingine kabisa.