Hapa kama script inamzingua vile Monalisa,lakini sasa atafanyaje na ndo hiyo ajira yake na huyu mama yangu naye anaandaa hapo script kazi kwenye kukariri halafu mkononi ana pesa dah! sijui mchaga.
Tuesday, November 8, 2011
PALE FILAMU ZINAPOTURUDISHA DARASANI
Unaweza kuhisi kwamba pindi unapovaa joho ama la kuhitimu kidato cha nne cha sita ama joho la heshima la chuo kikuu kwamba umemaliza kila kitu kuhusu kusoma dah!!! katika tasnia ya filamu mambo yanarejea kulekule kusoma kama kawaida. halafu mbaya zaidi ukiwa muhusika mkuu kuna kitu kinaitwa SCRIPT wanaoifahamu lugha vizuri wanasema ni mswada,mh!! yaani hapo ni zaidi ya darasa,kama ulikuwa hauna mazoea ya kukaririri 'what is biology,what is civics' sasa huku hakuna ujanja lazima ukaririri kwanza ndo uende mbele ya kamera,halafu huku hakuna cha kuangalizia ukithubutu kuangalizia kamera inakuumbua kwa hiyo lazima ukariri,aliyekwambia unaweza kuielewa script nani??? labda kama hiyo filamu umetunga mwenyewe kichwani,asikwambie mtu jamani script haina cha mzoefu


Hapa kama script inamzingua vile Monalisa,lakini sasa atafanyaje na ndo hiyo ajira yake na huyu mama yangu naye anaandaa hapo script kazi kwenye kukariri halafu mkononi ana pesa dah! sijui mchaga.
Hapa kama script inamzingua vile Monalisa,lakini sasa atafanyaje na ndo hiyo ajira yake na huyu mama yangu naye anaandaa hapo script kazi kwenye kukariri halafu mkononi ana pesa dah! sijui mchaga.
Friday, November 4, 2011
MONALISA NA KANUMBA WAINUSA HOLLYWOOD

Dah!! kama utani vile mwanadada mashuhuri katika tasnia ya filamu hapa bongo ambaye anatamba mkononi na tuzo yake ya msanii bora wa kike mwaka jana Yvonne Cherryl ali maarufu kama Monalisa pamoja na pacha wake katika tuzo kwa upande wa wanaume Stevene Kanumba,juhudi zao katika sanaa zinazidi kuzaa matunda huku wakipasua anga zaidi kimataifa na sasa wapo nchi iliyojaa vipaji vya sanaa ya maigizo Ghana. Hawajaenda kula bata kama wengi wanavyodhani bali wameenda kikazi zaidi huku wakiiwakilisha vyema afrika mashariki miongoni mwa vichwa vingine kutoka nchi mbalimbali tayari kwa kupakua mzigo wa maana.
Tuesday, November 1, 2011
MONALISA ABADILI DINI
Hiyo heading huenda imekushtua sana....... hapana usishtuke mbona kawaida kwani wangapi wamebadili dini na bado wanapeta??? kwani dhambi jamani. Hapana jamani alikuwa anatania tu,mwanadada mashuhuri ambaye anakaribia kuitwa nguli katika tasnia ya filamu bongo Yvonne Cherry yupo mzigoni na muda wowote kuanzia sasa msubiri hapo nyumbani kwako katika mzigo mpya anaoupiga na mtaalamu mwenzake Lucie Komba. Jina la picha naweka kapuni lakini mwanadada Monalisa hapo kati akiitwa Salma binti Sudi amevaa uhusika wa kiislamu na kubutua hiyo filamu ambayo bila shaka hajaharibu kitu chochote kama kawaida.
unaweza ukaamini yeye ndo kamvisha hili hijabu mwanadada binti wa Komba najua huwezi kuamini mtazame hapa chini.

hii ilikuwa siku ya kwanza....kwa behind the scene nyingine endelea kufatilia blog hii hadi mwisho wa mchezo
hii ilikuwa siku ya kwanza....kwa behind the scene nyingine endelea kufatilia blog hii hadi mwisho wa mchezo
Monday, October 31, 2011
TUWE SAUTI YAO
Naamini hawawezi kusikika hata wakizipaza sauti zao juu sana,si tu kwa sababu sauti zao ziko chini HAPANA ila watanzania wameziba masikio yao wasiweze kuwasikia na kuwasaidia. Hebu kuwa wa kwanza kufungua masikio yako na kumsikikliza bibi huyu akilia kwa uchungu mkali analia kilio cha upendo,upendo wake unasababisha chozi lake limdondoke. Hana uwezo mkubwa sana lakini ana upendo,kipato chake ni duni lakini bado anahitaji kusaidia wengine,kubwa zaidi ni MLEMAVU lakini hilo halimkatishi tamaa,kutana na bibi huyu katika show malidhawa itakayokujia hivi karibuni. Je unaamini kwamba waweza kuwa mlemavu lakini bado ukawasaidia wengine wasiojiweza zaidi yako??
"mabadiliko huanzia kwa mmoja na hatimaye dunia nzima" anaonekana akisema mama huyu mlemavu ambaye ana jukumu linalomzidi uzito....vuta subira utamfahamu kiundani hivi karibuni.......
Thursday, October 20, 2011
MONALISA KUISHANGAZA TANZANIA NA DUNIA!!!
Msanii maarufu wa filamu hapa nchini anayewika hadi nchi za watu huku akijivunia kuwa muigizaji bora wa kike kipindi flani hivi sasa anakuja kivingine kuikamata Tanzaniana mipaka yake.....unahisi anaandaa filamu mpya bada ya kutamba naBinti Nusa iliyompa tunzo??...au unadhani anaandaa muziki???...mimi na wewe hatufahamu kama ndo ameamua kuacha sanaa ya filamu ili kuishangaza Tanzania au vipi,yeye mwenyewe hakufunguka sana ila alisema kaneno flani hivi nami namnukuu
"coming soooon!!!!!!" hebu tazama hapa akiwa bize nyuma ya camera katika hizo location hapa juzi kati.

hapa mama na mwana...Monalisa akiwa anaandika masuala kadhaa soon baada ya kufika location.
"coming soooon!!!!!!" hebu tazama hapa akiwa bize nyuma ya camera katika hizo location hapa juzi kati.
hapa mama na mwana...Monalisa akiwa anaandika masuala kadhaa soon baada ya kufika location.
I AM BACK
Ni siku nyingi sana nimekuwa kimya katika ulimwengu huu wa blogu lakini sasa nimerejea mzima mzima kuendelea kuwa nanyi karibu,kuwajuza nanyi kunijulisha mambo kadha wa kadha katika tasnia hii ya filamu zetu za kibongo. Fuatana nami upya tena kama zamani........hebu ngoja niwapigie namba zenu kama mnapatikana maana na nyie kwa kubadili namba siwawezi
Saturday, March 5, 2011
Nimetembelea Kambi ya Yatima na Wazee wasiojiweza na kula lunch pamoja nao

Nungwi-Kigamboni kwenye kambi ya yatima na wazee wasiojiweza zamani ikifahamika kama kambi ya wenye Ukoma ndiko nilipotembelea weekend hii na kula lunch pamoja nao.Chakula kilichopikwa na sisi wenyewe katika kikundi chetu cha wanawake cha Hybiscus

Hapa tukipata msosi na kupiga story mbili tatu na bibi huyu ambaye ni mgonjwa na anayeishi kambini hapo,alifurahi sana.
Chakula bila maji?Nikiwahudumia watoto
Huyu mtoto alinitia majonzi na kunidondosha chozi....Ni yatima na hapo kambini yupo yeye na wadogo zake wawili.Alinipenda sana nami nimempenda sana pia

Akiendelea kunielezea mkasa wake
ITS TIME TO GO,Tukawaachia na zawadi ndogo ya vyakula tulivyojaaliwa kununua.michele,unga,mafuta,sabuni na vitu kama hivyo ili viweze kuwafariji na kufahamu kuwa kuna watu mahala fulani ambao tunaguswa kwa namna moja au nyingine na matatizo yao.
Subscribe to:
Posts (Atom)