Monday, December 27, 2010

NO.6 TUKIO LILILONISHTUSHA

Siku chache kabla ya Birthday yangu,wakati tunatoka kwenye Sherehe ya Kitchen Party ya rafiki yetu wa kanisani,mimi na mama yangu tulipata ajali.Ni kitendo cha dakika tu lakini kimedumu akilini mwangu hadi leo hii.Dereva aliyekuwa nyuma yetu alikuwa speed ya ajabu,na alipofika kwenye Roundabout ya Mlimani City, maeneo ya MWENGE,DAR ES SALAAM gari ilimshinda akaja kutugonga kwa nyuma nilipokuwa.gari yetu ikagonga ukuta wa barabara na kuzunguka kurudi tulipotokea,naye akaja tena kutugonga ubavuni,ubavu ule ule nilipokuwa nimekaa.Hatukuamini kama tumetoka salama,hakuna mtu aliyeumia japo mbavu na kichwa kiliuma sana kesho yake na ni kwa ajili ya mshtuko tu.Namshukuru sana MUNGU kwa kutuokoa katika ajali hiyo.Ni wengi wanaopata ajali na hawaponi,mimi ni nani nitoke mzima?Ni kwa REHEMA na MAPENZI yake MUNGU.



Naikumbuka sana siku hiyo,ilikuwa tarehe 8 ya mwezi wa 8.

No comments:

Post a Comment